1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Santa Domingo. Umoja wa Ulaya wataka kufunga mikataba na Latin Amerika.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8g

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anakamilisha ziara yake ya siku tano katika Latin Amerika kwa mazungumzo katika jamhuri ya Dominika.

Pamoja na mratibu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja Javier Solana na mawaziri kutoka mataifa mengine ya umoja wa Ulaya , Steinmeier anajadili kuhusu mikataba imara ya kiuchumi na kisiasa na mataifa ya Amerika ya kusini.

Umoja wa Ulaya ungependa kukamilisha makubaliano ya kibiashara na kundi la mataifa hayo. Kwa upande wake, mataifa hayo yameahidi kuunga mkono juhudi za umoja wa Ulaya za kulinda mazingira duniani.