1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya amani ya kimataifa

21 Septemba 2009

Tarehe 21 Septemba kila mwaka inaadhimishwa duniani kote siku ya kimataifa ya amani. Siku hii ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani imetangazwa na UN kuanzia mwaka 2001.

https://p.dw.com/p/JlPE
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki MoonPicha: AP

Kwa hivi sasa kuna mizozo 345 duniani kote. Jumuiya ya kimataifa hata hivyo inachukulia mizozo michache kwa dhati kama Afghanistan , lakini mingi ya mizozo imesahaulika.

Je dunia imekuwa ya amani tangu pale yalipofanyika maadhimisho ya mwaka wa saba yaliyofanyika mwaka mmoja ulipita tangu siku hii kuanza kuadhimishwa na umoja wa mataifa. Katika swali hili hakuna jibu sahihi. Hususan kwa wakati huu. Takwimu za mizozo kwa mwaka huu 2009 zilizokusanywa na taasisi za uchunguzi zitatolewa mapema mwezi wa Desemba. Na pia jibu la swali lililoulizwa hapa linaweza kujibiwa kwa njia tofauti. Kila jibu litategemea aina ya mzozo uliofanyiwa uchunguzi.

Tathmini ya mizozo

Taasisi ya utafiti wa mizozo ya kimataifa katika chuo kikuu cha Heidelberg kwa ajili ya kipimo chake cha mizozo ya dunia imeteua mmoja kati ya mizozo tofauti kwa mwaka 2002. Taasisi hiyo inaelezea kuhusu ngazi tano kuanzia mwanzo kabisa wa mzozo, mzozo unapoanza ambapo hakuna mapambano ya silaha, hadi inapofikia hatua ya kupanga na kuweka utaratibu wa mapambano, na kufikia hadi kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa msingi wa tofauti ya tathmini hizi , kama inavyoeleza taasisi hiyo, mwaka 2008 kumekuwa na mizozo mingi kuliko miaka iliyopita, kama anavyoeleza Lotta Mayer,''Tumeorodhesha kwa jumla mizozo 345. Hiki ni kiasi kikubwa kuliko wakati wowote ambao tulianza kufanya utafiti.''mfanyakazi wa taasisi hiyo.

Kiwango hicho kikubwa cha mizozo 345 katika mwaka 2008 kinaakisi sio tu hali mbaya ya kuongezeka kwa hali isiyokuwa ya amani duniani , lakini huenda ni hali halisi.

Kwamba hali imekuwa bora zaidi katika miaka kumi iliyopita, na kwamba kwa hivi sasa tumepata uzoefu mkubwa zaidi wa mizozo katika maeneo ya ndani zaidi ya dunia yetu, wakati katika miaka ya 50 na 60 kulikuwa na matatizo makubwa zaidi, hususan katika maeneo mbali mbali ya Afrika.

Vita vimezidi

Gaza Stadt Rauch steigt auf Israelische Militäroperation im Gaza-Streifen Überlagernde Grafik Amnesty International
Ukanda wa Gaza ukifuka moshi mwezi Januari 2009Picha: AP/DW-Grafik

Katika hali ya kutokuwa na usalama kutokana na kuzuka duniani kote kwa mizozo mingi ni utaratibu uliowazi wa aina ya mizozo tunayoifahamu. Kituo hicho cha utafiti katika chuo kikuu cha Heidelberg kimegundua.

Ikilinganishwa na mwaka 2007 , dunia mwaka 2008 imekuwa na matatizo makubwa ya kivita. Kiwango cha mizozo kimepanda kutoka 32 hadi 39, na katika mizozo hii 39 kuna vita vipya. Katika mwaka uliopita kulikuwa na mizozo sita tu. Pamoja na hiyo kuna kile kinachoitwa mizozo 95. Hii ni mizozo ambayo hulipuka mara kwa mara. Mizozo mingine 211 si ile ya mapambano.

Katika miezi mitatu iliyopita baada ya maadhimisho ya mwaka wa saba wa amani wa umoja wa mataifa Septemba 2008 kulikuwa na vita vya Gaza kati ya majeshi ya Israel na Hamas ambapo ulikuwa mzozo mwingine mpya mkubwa wa matumizi ya silaha. Hakuna mzozo ambao unaweza moja kwa moja kuwa umetulia. Kwa mwaka 2009 taasisi hiyo ilitarajia maendeleo duniani kote katika miezi tisa na nusu ya mwanzo hadi hii leo ambapo ni maadhimisho ya nane ya amani duniani kuwa mizozo mikubwa haitabadilika kuliko ilivyokuwa mwaka 2008.

Mwandishi Andreas Zumach/ ZR / Sekione Kitojo

Mhariri :Mwadzaya thelma