1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Siku ya Nelson Mandela"

18 Julai 2010

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela leo anatimiza miaka 92, huku ulimwengu ukisherehekea kwa mara ya kwanza, "Siku ya Nelson Mandela Duniani" kwa heshima ya kiongozi huyo.

https://p.dw.com/p/OOD8
Former South African president Nelson Mandela waves as he leaves his hotel in London,Thursday, June 26, 2008. Mandela is in the UK to celebrate his 90th birthday which will see a concert in his honour at Hyde Park with the proceeds going to his 46664 charity. (AP Photo/Simon Dawson
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.Picha: AP

Viongozi wa kimataifa na watu wa kawaida nchini Afrika Kusini na nje ya nchi hiyo, wameahidi kujitolea kuhudumia jamii kwa dakika 67 katika ishara za kuadhimisha miaka 67 ya kiongozi huyo kushughulikia harakati za kisiasa.

Mwaka 2009, Umoja wa Mataifa uliamua kuitambua tarehe 18 Julai - siku alizozaliwa mzee Mandela, kama "Siku ya kimataifa ya Nelson Mandela" na itakuwa ikisherehekewa kote duniani. Kwa mujibu wa familia yake, kiasi ya watoto 100 kutoka vijiji vilivyo karibu na kule alikozaliwa, watakuwa nae leo hii

Former South African President Nelson Mandela waves as he is driven across the field during the closing ceremony ahead of the World Cup final soccer match between the Netherlands and Spain at Soccer City in Johannesburg, South Africa, Sunday, July 11, 2010. (AP Photo/Martin Meissner
Nelson Mandela akiwapungia mkono mashabiki wa kandanda kabla ya fainali ya Kombe la Dunia kati ya Uhispania na Uholanzi mjini Johannesburg.Picha: AP

Tangu kuondoka madarakani, Mandela amejitokeza hadharani mara chache tu. Juma lililopita alikwenda kwenye uwanja wa michezo wa Soccer City mjini Johannesburg, kuwapungia mkono mashabiki wa kandanda kabla ya kufunguliwa mchezo wa fainali wa Kombe la Dunia, lakini hakubakia kutazama mchezo kwa sababu ya hali yake dhaifu ya afya.

Mwandishi: Nyanza,Halima/AFPE

Mhariri: P.Martin