1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIRTE: Gadafi akutana na viongozi wa mataifa ya kiarabu

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYY

Rais wa Libya Muamar Ghadafi amefanya mkutano na viongozi wa mataifa ya kiarabu kutoka Algeria na Misri kudurusu maendeleo katika Mashariki ya Kati na Afrika.

Kwa mujibu wa afisa wa Libya ambaye hakutaka jina lake litajwe, rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria na Hosni Mubarak wa Misri wamehudhuria mkutano huo uliofanyika mjini Sirte, Libya, lakini akasita kuwataja viongozi wengine walioshiriki pia katika mazungumzo hayo.

Marais wa Sudan, Tunisia na Yemen wanatarajiwa pia kuhudhuria mkutano huo, lakini afisa wa serikali mjini Sanaa amesema Yemen haitashiriki kwenye mkutano huo.

Mkutano huo unaofanyaika siku chache kabla mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia na mkutano wa jumuiya ya nchi za kiarabu uliopangwa kufanyika mjini Riyadh Saudi Arabia mwezi Machi mwaka huu, unatarajiwa pia kuzungumzia hali ya jimbo la Darfur nchini Sudan na nchini Somalia.