1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SOFIA:Wahudumu 6 wa afya wawasili kwao Bulgaria

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfl

Manesi 5 na daktari mmoja waliohukumiwa kifungo cha maisha nchini Libya kwa mashtaka ya kuwaambukiza watoto 400 virusi vya Ukimwi wamewasili nchini mwao Bulgaria.Wahudumu hao wa afya wanarejeshwa kwao baada ya mazunfumzo kati ya maafisa wa serikali ya Libya na Kamishna wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Benita Ferrero –Waldner.Mazungumzo hayo ya jana yaliungwa mkono na mkewe rais wa Ufaransa Bi Cecilia Sarkozy.

''Tunaweza kusema uamuzi wa serikali ya Libya ni uamuzi wa ki utu na kwa kweli unatokana na juhudi za pamoja za wanachama wengi wa Umoja wa Ulaya na hasa kwa leo hii,Ufaransa.''

Wahudumu hao walikuwa wanazuiliwa jela nchini Libya tangu mwaka 99.Mwanzo walipewa hukumu ya kifo ambayo ilibadilishwa wiki jana baada ya Baraza la Mahakama kuu kufikia makubaliano ya kuwafidia familia za watoto walioambukizwa.Kwa mujibu wa wataalam maambukizi hayo yalisababishwa na usafi duni katika hospitali walimokuwa wakifanyia kazi.