1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STOCKHOLM : Mkutano wa Maji wafunguliwa

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZU

Katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa kuhusu maji Waziri Mkuu wa Sweden Frederik Reinfeldt ametowa wito wa kushinikizwa zaidi kwa Marekani,China na India kushughulikia suala la kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.

Amesema Umoja wa Ulaya umetimiza dhima muhimu katika mchakato wa kushughulikia changamoto za kimazingira na kupunguza utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira.

Kiongozi huyo wa Sweden alikuwa akifunguwa mkutano wa Wiki ya Maji Duniani mjini Stockholm ambapo zaidi ya wataalamu 2,500 kutoka duniani kote wanatazamiwa kujadili vipi watu wengi zaidi wanavyoweza kupatiwa uwezo wa kujipatia maji safi ya kunywa.

Reinfeldt amesema watu wapatao 34,000 hufariki kila siku kutokana na magonjwa yanaohusiana na ukosefu wa maji au mifumo ya usafi.

Hata hivyo amesema kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2002 asilimia 79 ya idadi ya watu duniani walikuwa na maji safi ya kunywa kutoka asilimia 71 iliokuweko kabla ya hapo.