1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stoiber apata kazi mpya Umoja wa Ulaya

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJVl

Waziri Mkuu wa zamani wa jimbo la kusini mwa Ujerumani la Bavaria amepata kazi mpya.

Edmund Stoiber amekuwa mshauri wa Umoja wa Ulaya katika suala la kupunguza urasimu katika umoja huo wa nchi wanachama 27.Stoiber atakuwa mwenyekiti wa wataalamu ambao kazi yao itakuwa ni kuzibainisha sheria na taratibu zisizokuwa na ulazima wa kuwepo.

Umoja wa Ulaya unatarajia kupunguza gharama za urasimu kwa asilimia 25 kufikia mwaka 2012.