1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN:Iran yamwachia kwa dhamana msomi wa kimarekani

21 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBX4

Iran leo imemwachia msomi wa Marekani mwenye asili ya nchi hiyo, iliyokuwa ikimshikilia toka mwezi wa tano kwa makosa ya kiusalama.

Taarifa kutoka Teheran zasema kuwa Msomi huyo Haleh Esfandiari ameachiwa kwa dhamana ya dola 320,000.

Hakuna taarifa zaidi juu ya kuachiwa kwake, ambapo mapema Marekani ilisema kuwa imepokea kwa furaha taarifa za kutaka kuachiwa kwa msomi huyo.

Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani Gordon Johndroe akizungumza huko Montebello Canada aliko na rais Bush katika mkutano na wakuu wa Canada na Mexico, amesema kuwa uamuzi huo unatia moyo.

Msomi huyo mwanamke mwenye umri wa miaka 67 alikamatwa mwezi wa tano mwaka huu kwa tuhuma za kuifanyia ukachero Marekani kwa nia ya kutaka kuuangusha utawala wa Iran