1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yaendelea na urutubishaji wa uranium

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyd

Iran imesema inaendelea na kazi yake katika kinu cha kurutubisha madini ya uranium na imetia gesi katika mitambo yake kwa mara ya pili.

Shirika la habari la ISNA limemnukulu afisa wa Iran ambaye hakutajwa jina lake akisema gesi ilitiwa kwa mara ya kwanza kwenye mitambo ya kurutubisha uranium wiki iliyopita na tayari matokeo yaliyotarajiwa yamepatikana.

Iran ilithibitisha mnamo Jumatano wiki hii kwamba imeweka kifaa kipya cha kurutubisha uranium.

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, ameilinganisha azma ya Iran kutaka kumiliki nyuklia na vitisho vyake kwa Israel na sera za Ujerumani chini ya utawala wa manazi.

Olmert ameyasema hayo leo mjini Jerusalem wakati wa sherehe ya kitaifa ya kuadhimisha mauaji ya halaiki ya wayahudi.