1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN : Wanamaji 15 wa Uingereza washikiliwa Iran

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCG2

Iran imemwita mwanadiplomasia mkuu wa Uingereza alieko Tehran kupinga kile ilichokieleza kuwa kuingia kinyume na sheria kwa wanamaji wa Uingereza katika eneo la bahari la Iran.

Wanamaji na mabaharia 15 wa Uingereza wamechukuliwa chini ya mtutu wa bunduki na wanajeshi wa Iran katika Ghuba ya Uajemi lakini Uingereza inasema wanamaji hao walikuwa kwenye bahari ya Iraq.

Serikali ya Uingereza inadai kurudishwa kwa salama kwa wanamaji wake hao na imemwita balozi wa Iran mjini London kuelezea kisa hicho.

Doria ya kijeshi ya Uingereza imepewa mamlaka ya kuzipekuwa meli kwenye eneo la bahari la Iraq chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa na kwa ruhusa ya serikali ya Iraq.