1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Israel yaregeza masharti ya kuvuka vituo vya ukaguzi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCe4

Israil imeanza kuregeza masharti ya kuvuka vituo vya ukaguzi katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Mwezi uliopita Waziri Mkuu wa Israil, Ehud Olmert alipokutana na Rais wa Palestina Mahmud Abbas, aliahidi kuchukua hatua kadhaa ili kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili.

Waziri wa Ulinzi wa Israil Amir Peretz alikuwa amesema kuwa serikali yake ina mpango wa kuondoa vizuizi hamsini na tisa vya barabarani miongoni mwa vizuizi mia nne katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Raia wa Kipalestina wanaotembea katika eneo hilo hulazimika kupitia vituo vingi vya ukaguzi vilivyowekwa kwa lengo la kuwadhibiti wanamgambo.

Nako mjini Gaza, Msemaji wa chama cha Hamas amesema kuna ishara za matokeo mazuri katika mashauriano yanayoendelea kuhusu kuachiliwa huru mwanajeshi wa Israel anayeshikiliwa na kundi la wanamgambo wa Palestina.

Msemaji huyo hakutoa taarifa zaidi lakini alisema mashauriano hayo yameendelea vyema na huenda askari huyo, Gilad Shalit, akaachiliwa huru hivi karibuni baada ya Israil nayo kuwaachilia huru wafungwa wa Kipalestina.

Shalit alitekwa mjini Gaza mwezi Juni, hali iliyosababisha Israil kushambulia ukanda wa Gaza ambapo mamia ya wapalestina waliuawa.