1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Biashara ya pembe za ndovu kupigwa marufuku

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrf

Nchi za Kiafrika zimechukua hatua muhimu ya kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu. Kuambatana na makubaliano hayo,nchi za kusini mwa Afrika zitaruhusiwa mara moja kuuza pembe zilizorundikana ambazo zilipatikana kihalali.Pesa zitakazopatikana kutoka uuzaji huo,zitatumiwa kuhifadhi wanyama.Baada ya miaka tisa,ruhusa nyingine itatolewa kuuza pembe za ndovu. Makubaliano hayo yamepatikana mjini The Hague baada ya kuwepo mabishano makali ya siku kadhaa,katika mkutano wa Biashara ya Kimataifa ya Viumbe vilivyo Hatarini.