1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

The Hague. Kesi ya Seselj yaanza.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79G

Kesi ya uhalifu wa kivita inayomhusu mwanasiasa mzalendo wa Serbia Vojislav seselj imeanza katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague. Seselj anakabiliwa na madai ya mauaji , utesaji na kuchochea chuki wakati wa mzozo ambao ulisababisha kuvunjika kwa iliyokuwa Yugoslavia ya zamani katika miaka ya 1990.

Waendesha mashtaka wamesema kuwa alihusika katika mipango ya kuwaondoa kwa nguvu watu wasio Waserb kutoka katika maeneo ya Croatia na Bosnia. Amekana madai hayo. Kiongozi huyo wa chama chenye msimamo mkali cha Serbia mwenye umri wa miaka 53 alijisalimisha kwa mahakama hiyo mwaka 2003.

Seselj alikuwa mshirika wa karibu wa kiongozi wa Serbia Slobodan Milosevic, ambaye alifariki dunia akiwa kizuizini mjini The Hague mwezi March mwaka jana wakati akisubiri hukumu katika kesi yake ya uhalifu wa kivita.