1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI : Mzozo wa wauguzi wa kigeni kutatuliwa

11 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBst

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank –Walter Steinmeir na Kamishna wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Benita Ferrero- Waldner wamewasili mjini Tripoli kujaribu kutatua mzozo wa wanamatibabu wa kigeni waliohukumiwa kifo nchini humo.

Wanatazamiwa kukutana na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kujadili suala hilo la wauguzi watano wa Bulgaria na daktari wa Kipalestina waliokamatwa nchini humo tokea mwaka 1999.Hapo mwaka jana walipatikana na hatia ya kuwaambukiza viruis vya HIV kwa makusudi zaidi ya watoto 400 wa Libya.

Wanamatibabu hao wanasema hawana hatia na kwamba wamekirri tu kutenda uhalifu huo baada wa kuteswa.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na wanadiplomasia hao waandamizi wa Ulaya mtoto wa kiume wa Gaddafi Saif al Islam amesema matokeo ya juhudi hizo yatakuwa mazuri na kwamba wanatumai huo utakuwa mwanzo wa kulimaliza tatizo hilo.