1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uamuzi wa mahakama wazusha ghadabu kali nchini Misri

27 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/Ekkm

CAIRO

Jamaa za watu 1000 waliokufa baada ya ferry waliyokuwa wakisafiria kuzama mwaka 2006 nchini Misri wameghadabishwa na uamuzi wa mahakama hii leo ambapo mmiliki wa ferry hiyo amekutikana hana hatia.

Jamaa za wahanga wa ajali hiyo wamepamabana vikali na vikosi vya usalama huku wengine wakiwalaani majaji na mawakili waliohusika na kesi hiyo.

Mmiliki wa ferry hiyo ambaye ni mfanyibiashara tajiri anasadikiwa kuwa rafiki wa karibu wa wanasiasa kadhaa nchini Misri.

Mahakama hiyo pia imewaachilia huru watu wengine wanne waliokuwa wakifanya kazi katika ferry hiyo.Hata hivyo mahakama imemkutana na hatia nahodha wa meli nyingine kwa kushindwa kuisadia ferry hiyo na kumhukumu kifungo cha miezi sita jela.

Tume maalum iliyoundwa na bunge kuchunguza ajali hiyo iliilaumu kampuni ya Ferry kwa kusababisha ajali hiyo mbaya ikisema iliendelea kuitumia ferry hiyo licha ya kuwa mbovu.