1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Togo

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ft

Wapiga kura milioni tatu wa Togo wanateremka vituoni hii leo kulichagua bunge jipya.Watetezi zaidi ya elfu mbili kutoka vyama zaidi ya 32 vya kisiasa wanapigania viti 81 vya bunge.Hii ni mara ya kwanza kwa chama cha upinzani cha Umoja kwaajili ya mageuzi UFC kushiriki katika uchaguzi huo,tangu mageuzi ya kidemokrasi yalipoanzishwa nchini Togo miaka 17 iliyopita.Uchaguzi huu wa leo unaangaliwa kama kipimo kwa umashuhuri wa chama tawala cha-Muungano wa Umma wa Togo-RPT,baada ya muanzilishi wake,Gnassingbe Eyadema kufariki dunia, mwaka 2005.Wachunguzi 3500 wa kitaifa na kimataifa wanasimamia uchaguzi huo.Gnasingbe Eyadema aliitawala Togo kwa muda wa miaka 38.