1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi wa Dunia na mfumko wa bei ni mada zitazotawala mkutano wa G8 leo

Saumu Mwasimba7 Julai 2008

Bara la Afrika linamulikwa zaidi kuhusu suala la mfumko wa Bei

https://p.dw.com/p/EXR4
Rais wa Marekani Goerge Bush na waziri mkuu wa Japan Yasuo Fukuda wasema ipo haja suala la mabadiliko ya hali ya hewa litatuliwePicha: AP

Viongozi wa kundi la nchi nane tajiri kiviwanda duniani la G8 wanaanza hii leo mkutano wao wa siku tatu nchini Japan na masuala muhimu yakujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na uchumi wa dunia na kupanda kwa bei za vyakula na mafuta pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkutano huo pia unahudhuriwa na viongozi wa China,India,Brazil na Afrika Kusini miongoni mwa wengine.Viongozi wa Afrika wanaohudhuria mkutano huo wanatazamiwa kuzungumzia wasiwasi wao juu ya kuzidi kupanda kwa gharama za maisha hali ambayo imeongeza matatizo kwa watu maskini wa bara hilo.Aidha suala la hali ya kisiasa nchini Zimbabwe litajadiliwa ambapo viongozi wa G8 wanatazamiwa kulaani kwa pamoja kurudi tena madarakani kwa rais Robert Mugabe.Hali ya usalama imeimarishwa katika kisiwa cha kaskazini mwa Japan cha Hokkaido kwenye mji wa Toyako ambako mkutano huo unafanyika. Jana mamia ya waandamanaji walijitokeza katika barabara za mji wa Sapporo ulioko karibu na eneo la mkutano kuwashinikiza viongozi wa G8 kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya hali ya hewa,umasikini na kupanda kwa bei za vyakula duniani.