1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUgiriki

Ugiriki yaahidi msaada zaidi kwa visiwa vya Crete na Gavdos

Tatu Karema
2 Aprili 2024

Serikali ya Ugiriki imeahidi msaada zaidi wa kifedha na wafanyakazi kukisaidia kisiwa cha Crete na kisiwa kidogo jirani cha Gavdos kushughulikia ongezeko kubwa la wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya kutoka Libya

https://p.dw.com/p/4eK13
Wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika kwenye bahari ya Mediterenia wakiwa safarini kuelekea Ulaya mnamo Januari 28, 2022
Wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika katika bahari ya MeditereniaPicha: Pau de la Calle/AP/picture alliance

Baada ya ziara katika visiwa viwili vya Crete na Gavdos, waziri wa uhamiaji wa Ugiriki Dimitris Kairidis, alisema watazisaidia jamii za maeneo hayo na kuongeza kwamba kuna raslimali na njia za kutosha kufanikisha hilo.

Idadi ya wahamiaji yaongezeka visiwani Crete na Gavdos

Katika miezi ya hivi karibuni, visiwa vya Crete na Gavdos, vimeshuhudia ongezeko kubwa la wahamiaji lisilo la kawaida zaidi kutoka Misri, Pakistan na Afghanistan.

Soma pia:Wahamiaji 100 waokolewa pwani ya Ugiriki

Takwimu za walinzi wa Pwani ya Ugiriki, zinaonesha kuwa tangu mwezi Januari, zaidi ya wahamiaji1,180 waliwasili kwenye visiwa hivyo viwili, hili likiwa ongezeko kutoka idadi ya wakimbizi 686 waliowasili visiwani humo mwaka mzima wa 2023.

Visiwa vyote viwili vya Gavdos na  Crete, havina vituo vya kuwapokea wahamiaji.