1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugonjwa wa usubi ungali ukisambaa ulimwenguni

Christopher Buke16 Desemba 2006

Unatibika kwa urahisi lakini madhara yake makubwa.

https://p.dw.com/p/CHls

Nchi zaidi ya 35 zilizo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa usubi zimehimizwa kuongeza kasi ya kupambana na ugonjwa huo ili kuweza kuutokomeza.

Hii ni pamoja na kuweka mikakati mipya ya kuzuia, kutibu na kuwahamasisha wananchi wanaoishi kwenye maeneo ambayo yanashambuliwa na ugonjwa huu wachukue tahadhari ikiwa ni pamoja na kumeza dawa za kuzuia ugonjwa huu na mapema.

Mkutano huu kwa upande mwingine ulionesha utashi mkubwa wa kisiasa kutokana na kuwa hata watawala na wanasiasa walihudhuria na kutoa ahadi za kuendeleza mapambano dhidi ya adui usubi.

Ndio maana mkutano huo ukawaleta kwa pamoja mabingwa kutoka sekta za afya kutoka nchi mbalimbali, zaidi ya mawaziri 20, wasomi na wanasiasa kutoka zaidi ya nchi 25 zilizo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania binafsi ndiye aliufungua mkutano huo uliofanyika mwanzoni mwa mwezi wa Desemba 2006, naye akianisha madhara ambayo tayari yamesababishwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watanzania.

Kwa mujibu wa takwimu za mabingwa wa afya kwenye mkutano huo tayari mataifa 35, yanasumbuliwa na ugonjwa huo.

Mataifa 28 kati ya hayo ni ya ki-Afrika. Jumla ya watu wanaougua ugonjwa huo kote ulimwenguni hivi sasa wamefikia milioni 18.

Ugonjwa huu hutokana na minyoo aina ya onchecerca volvulus na kusambazwa na inzi weusi majike wadogo-wadogo mithiri ya mbu wajulikanao kama simulium. Mbu hawa huzaliana kwa wingi kwenye maeneo yenye vijito au mito yenye maji yatiririkayo kwa kasi.

Wadudu hawa wana uwezo wa kuruka hadi umbali wa kilometa 400. Waziri wa Afya wa Tanzania na maendeleo ya Jamii Profesa David Mwakyusa anasema licha ya kuwa wadudu hawa wana umbo linaloshabiriana sana na la mbu lakini tabia zao ni tofauti kabisa.

“Kwa sababu wao wanapendelea kuzaa kwenye miamba ambapo kuna maji yanapita haraka.

Ambapo hawa mbu wanaoeneza malaria kama unavyojua wanatafuta maji ambayo yametuama kwa hiyo katika maeneo ambayo kuna mito ambayo ina maji ambayo yana kwenda haraka ndo unawapata”. Anasema waziri na kuyataja maeneo ambayo wanapatik