1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhaba wa maji na ukame mkubwa waikabili China

12 Februari 2009

Maeneo ya kilimo yaathirika

https://p.dw.com/p/Gshj
Kuharibiwa maziwa kama hili la Dianchi 2007 ni moja wapo ya matatizo ya upatikanaji wa maji safi ya kunywa.Picha: picture-alliance/dpa

China inakabiliwa na janga kubwa la ukame kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miongo mitano iliopita, hali ambayo imesababisha uhaba wa maji nchini humo. Watu wengi katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu duniani wanatumia kwa kasi kubwa vyanzo vya maji yanayozidi kupungua na kusababisha ukame. Wataalamu wa Kichina na wa nchi za nje, wamekua wakionya mara kadhaa huku mito na maziwa yakiendelea kukauka na vima vya maji chini ya ardhi vikipungua, wakati mabadiliko ya hali ya hewa yakisababisha barafu kuyayuka katika kasi isiyowahi kuonekana hapo kabla.

Wakati huo huo, uharibu wa maji ni jambo linalozidi kwa kasi kubwa. Utafiti wa benki ya dunia kuhusiana na gharama ya hivi karibuni ya uharibifu wa mazingira nchini China, umeashiria kwamba China inakabiliana na changamoto kubwa katika kusimamia vyonzo vyake vaya maji ili kudumisha ukuaji uchumi katika miaka ijayo.

Tatizo la maji tayari linaigharimu China kiasi cha 2.3 asili mia ya pato jumla la taifa-ikiwa ni kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya dunia. zaidi ya watu milioni 300 katika maeneo ya mashambani hawana maji ya kunywa yalio safi na ya usalama na magonjwa miongoni mwa watoto kama kansa na kuharisha yanaongezeka .

Kiasi ya miji mikubwa 400 kati ya 660 nchini China ina ukosefu wa maji ya kutosha, wakati hali ikiwa ni mbaya zaidi katika miji mikubwa ya Beijing na Tianjin.Mji mkuu Beijing umekua na ukosefu wa mvua kwa zaidi ya siku 100 sasa huku mikoa 15 ikiathirika kutokana na ukame mbaya kuonekana kwa miongo kadhaa wakati wa msimu wa baridi.

Miji mikubwa mingi na mengine midogo, imetangaza hali ya hatari wakati mavuno katika hekari milioni 10 za ardhi ya kilimo ikiwa hatarini.Kwa hivyo China sio tu haina budi kulitatua tatizo la uhaba wa maji ambalo ni la muda mrefu lakini pia hali ya ukame.

China kwa wakati huu ina akiba ya maji ya 7 asili mia , inayotosha kukidhi mahitaji ya 20 asili mia ya idadi ya wakaazi duniani. Kwa kuwa sehemu kubwa ya akiba hiyo inakutikana kusini mwa nchi hiyo, eneo la kaskazini limo katika hali mbaya na ni huko inakokutikana theluthi mbili ya ardhi ya kilimo, ambako hutimika utaratibu wa umwagiliaji maji mashamba hutumika. Sehena kubwa ya maji hupatikana kutoka katika visima.

Wataalamu wanasema katika kukabiliana na changamoto hiyo, Benki ya dunia imependekeza marekebisho kabambe katika usimamizi wa matumizi ya maji nchini China, pakiwemo ufundi wa kuweka akiba na kurekebisha bei ya maji,ufafanuzi wazi wa haki za kumiliki maji na sheria kali za hifadhi ya mazingira.

Mohammed AbdulRahman/IPS