1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhuru wa Kosovo hautotangazwa kabla mwezi Aprili

14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbV0

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya utapitisha uamuzi wake kuhusu hatima ya Kosovo,baada ya uchaguzi wa rais wa Serbia utakaofanywa mwisho wa mwezi Januari. Kamishna wa Upanuzi wa Umoja wa Ulaya,Olli Rehn amesema,suluhisho la Kosovo linatazamiwa kupatikana majira haya ya baridi au mwanzoni mwa majira ya kuchipua.

Rehn amenukuliwa akiwaambia wabunge wa Umoja wa Ulaya kuwa amehakikishiwa na waziri mkuu mteule wa Kosovo,Hashim Thaci kuwa hatotangaza uhuru wa Kosovo,kabla ya mwezi wa Aprili na ataziarifu nchi za Magharibi kuhusu hatua hiyo.

Wakosovo wenye asili ya Kialbania ambao ni wengi, wanataka uhuru wao kutoka Serbia,lakini serikali mjini Belgrade inashikilia kuwa jimbo hilo lililojitenga linaweza kuwa na mamlakahuku likibakia sehemu ya Serbia.