1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi bado ni kikwazo

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChHH

JERUSALEM

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina wamekuwa na mazungumzo mjini Jerusalem lakini wameshindwa kutatuwa mvutano juu ya mipango ya Israel kujenga makaazi mapya ya walowezi wa Kiyahudi mashariki mwa Jerusalem.

Hata hivyo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendelea na mazungumzo ya amani yaliofufuliwa upya.Hiyo ni mara ya kwanza kwa viongozi hao kukutana tokea kufanyika kwa mkutano wa amani uliofanyika nchini Marekani mwezi uliopita.

Kwenye mazungumzo hayo ya jana Abbas ameitaka Israel isitishe harakati zote za kujenga makaazi ya walowezi wa Kiyahudi kama inavyotakiwa na kile kinachojulikana kama mpango wa ramani ya amani Mashariki ya Kati.Lakini afisa wa serikali ya Israel amesema Olmert ameendelea kutetea mipango ya ujenzi wa makaazi hayo.

Mipango hiyo imewekea kiwingu mazungumzo hayo ya amani ambayo yalifufuliwa tena baada ya kukwama kwa miaka saba.