1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa, New York. Venezuela na Guatemala zatoka sare umoja wa mataifa.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0y

Baada ya duru 13 za upigaji kura katika siku moja kushindwa kupata mshindi kati ya nchi ya Guatemala na Venezuela kuhusiana na kuichagua nchi mojawapo kati ya hizo kuingia katika baraza la usalama la umoja wa mataifa , baraza kuu la umoja wa mataifa limeahirisha kura hiyo hadi wiki ijayo ili kutoa nafasi kwa wanadiplomasia kutatua suala hilo.

Baraza hilo hadi sasa limefanya duru 35 za upigaji kura katika muda wa siku tatu, huku kura za kila nchi zikiwa hazionyeshi hatua yoyote ya ushindi.

Upigaji kura utaendelea hadi nchi moja itakapochaguliwa kutumikia kipindi cha miaka miwili kuanzia Januari mosi mwaka ujao.