1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wawashambulia waasi wa M23

13 Julai 2012

Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa na lile la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametumia helikopta kuwashambulia dhidi ya kundi la waasi la M23 baada ya waasi hao kutishia kuuvamia mji wa mashariki wa Goma.

https://p.dw.com/p/15XE9
Waasi wa M23 mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Waasi wa M23 mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Picha: picture-alliance/dpa

Helikopta za jeshi la nchi hiyo aina ya FARDC zilionekana katika maeno ya vijiji vya Nkokwe na Bukima, eneo ambalo kundi la waasi linalojiita M23 linasadikiwa kuweka kambi, wakati jeshi la Umoja wa Mataifa walitumia helikopta aina ya M124 na M125 zilizokuwa zikiedeshwa na marubani kutoka Ukraine.

Mashambulizi hayo yamekuja baada ya Rwanda na Kongo kukubaliana jana kuacha mapigano hayo.

Chanzo cha habari kutoka Umoja wa Mataifa kimesema kuwa walilazimika kutumia bunduki kuwatawanya waasi hao waliosemekana kutishia kusababisha machafuko katika mji wa Goma.

Waangalizi wa amani nchini Kongo kutoka Umoja wa Mataifa wanaodai kuwa waasi hao wanatokea Rwanda awali waliweka kambi katika eneo la Kivu ya Kaskazini, lililoko Mashariki mwa Kongo

Waasi wataka mazungumzo na serikali

Hata hivyo waasi hao wanadai kuwa hawakuwa na lengo la kuuteka mji huo bali wanatishia tu ili kuilazimisha serikali ya Kinshasa izungumze nao.

Mji wa Goma, mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mji wa Goma, mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Picha: AP

"Jeshi la serikali linavamia upande wetu, ingawa hawajui tuliko, hakuna matatizo, lakini sisi hatujali", alisema kanali wa kundi la waasi

Kundi la waasi la M23 linaloongozwa na Bosco Ntaganda lilipewa jina hilo baada ya kushindikana kwa makubaliano ya amani, Machi 23, 2009.

Ntaganda pia anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa tuhuma za kuwateka watoto wadogo na kuwatumia kama maaskari katika kundi lake la waasi.Hata hivyo, mwezi machi mwaka huu alilikimbia jeshi na kuanzisha vurugu katika eneo Kivu ya Kaskazini lililo mashariki mwa Kongo

Mwaka 2009, Ntaganda alikubaliwa kujiunga na jeshi la Kongo na kupewa cheo cha Jenerali. Hata hivyo, mwezi machi mwaka huu alilikimbia jeshi na kuanzisha vurugu katika eneo Kivu ya Kaskazini.

Mtuhumiwa mwingine ,kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa Union of Congolese Patriots, Thomas Lubanga, alihukumiwa wiki iliyopita kifungu cha miaka 14 jela na ICC.

Mwandishi: Flora Nzema/AFPE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman