1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya baada ya kuanguka serikali ya Czech

25 Machi 2009

Vipi usuhuba na Umoja wa Ulaya ?

https://p.dw.com/p/HJWn
Mirek TopolanekPicha: AP

Kuangushwa kwa waziri-mkuu wa Jamhuri ya Czech, Topolanek,kutokana na kuwa nchi hiyo ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya,kuna athari zake zinazoenea ulaya nzima.Serikali yake mjini Prague,hatahivyo, kwa sasa inaendelea kuongoza shughuli za serikali na hivyo haina wasi wasi.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Czech, Mirek Topolanek alieangushwa madarakani jana kwa kura ya kutokua na imani nae ,aliwasili leo binafsi katika Bunge la Ulaya mjini Strassvurg,Ufaransa kana kwamba nyumbani hakiujatokea kitu.Risala alitaka kutoa ifahamike-nayo ni kuwa licha ya msukosuko wa serikali,Umoja wa Ulaya usihofie kuzuka athari zozote upande wake.Hata katika kipindi cha mpito,serikali ya Bw.Topolanek itaendesha shughuli zake kama mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya kama ilivyopangwa hadi mwishoni mwa Juni muda wake utapomalizika.

Kiongozi wa kundi la wabunge wa kisoshalist katika Bunge la Ulaya Martin Schulz alisema,

"Kuhudhuria hapa leo asubuhi,kunaonesha kuwa wewe ni mtu uliovinjari kabisa."

Bw.Toplanek akakabili swali ikiwa mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya,jamhuri ya czech ina mipango gani hadi kipindi chake kumalizika.

Hakutaka afahamike kama mtu aliefungwa mikono na hawezi kutenda.Jamhuri ya Czech, alieleza waziri-mkuu huyo wa mpito inakusudia kutimiza jukumu lake.

Na wasemaji wengi leo katika Bunge hilo la Ulaya ,walionesha ni tayari kuendelea kushirikiana na Jamhuri ya Czech kana kwamba hakuna mabadiliko:

"Tunamuungamkono waziri mkuu wa Jamhuri ya Czech kukamilisha kwa mafanikio kipindi chake cha uwenyekiti."Alisema Bw.Pottering.

Ni kwa muda mfupi tu waziri mkuu wa Czech alizusha fadhaha bungeni.Aliwatuhumu wasocial democrat nchini mwake kuchochea msukosuko uliozuka.Hii ikamfanya mwenyekiti wa kundi la vyama vya kijamaa katika Bunge hilo la ulaya Martin Schulz kumjibu: "Topolanek hapaswi kulitumia bunge la ulaya kwa siasa za ndani za nchi yake."

Mbali na patashika hii,Tume na Bunge la Ulaya zinachukulia kuwa serikali mjini Prague itaendelea na kazi zake kama mwenyekiti wa umoja wa Ulaya. Rais wa Jamhuri ya Czech, Klaus ,aweza kupitisha wakati hadi kutoa jukumu nani aunde serikali mpya .Hata Upinzani mjini Prague umeridhia kumuachia waziri mkuu Topolanek kuiwakilisha Jamhuri ya Czech hadi kipindi cha urais kimepita.

Wasi wasi mjini Brussels, makao makuu ya Umoja wa Ulaya upo ni baada ya kumalizika kipindi hicho.Toplanek anaelemea Umoja wa Ulaya ,lakini yawezekana wakosoaji wa Umoja huo katika chama chake nao wakapata nguvu mpya .Kwani, katika Jamhuri ya Czech, Mkataba wa mageuzi wa UU -mkataba wa Lisbon,bado haukuidhinishwa.

Muandishi :Ramadhan Ali

Mhariri: Mohammed Abdulrahma