1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa ulaya wakubaliana juu ya sera moja kuhusu uhamiaji

8 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EY31

CANNES

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulalya wamekubaliana juu ya kuwa na sera ya pamoja katika kukabiliana na uhamiaji haramu katika nchi zote 27 wanachama wa Umoja huo.Mawaziri wanaokutana mjini Cannes Ufaransa wamezungumzia matumaini yao kwamba mpango wao juu ya uhamiaji na ukimbizi huenda ukakamilika kufikia mwezi Oktoba.Mpango huo unaweka wazi sheria za Umoja wa Ulaya katika kudhibiti uhamiaji na kupamabana na uhamiaji haramu.Waziri wa mambo wa ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble amesema kwamba Umoja wa Ulaya hauna budi kuchukua hatua hiyo kwasabubu hauwezi kuwa ngome ya wahamiaji haramu.Mpango huo hata hivyo umekosolewa vikali ndani na nje ya Umoja wa Ulaya.Hapo jana mjini Cannes polisi wa Ufaransa waliwakamata kwa muda wapiga picha wa televisheni ya Dw waliokuwa wakipiga picha maandamano ya kupinga sera za Umoja wa Ulaya kuhusu uhamiaji.