1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waonya Kenya kuwa endapo mgogoro wa kisiasa hautapata ufunzi itasita kuipa msaada

15 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CphS

NAIROBI:

Maofisa wa Umoja wa Ulaya wamesema kuwa msaada ya Umoja huo kwa Kenya unaweza ukazuiliwa ikiwa juhudu za upatanishi ili kutafuta suluhu ya mgogoro wa sasa wa kisiasa zitashindwa.

Umoja wa Ulaya ambao ndio unafadhili fadhili Kenya kwa kiwangi kikubwa , ulitoa Euro millioni 290 kati ya mwaka wa 2002 na 2007.Uchaguzi wa urais unaogombaniwa umezisha juhudi kadhaa za kimataifa za upatanishi.Miongoni mwa juhudi hizo ni za aliekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa-Kofi Annan amabe anatarajiwa kuwasili huko leo jumanne.Hata hivyo waziri mmoja na mshirika wa karibu wa rias Mwai Kibaki tayari amekataa upatanishi wa Annan.Kwa mda huohuo waKenya wanajitayarisha kwa siku tatu za maandamano ya kitaifa ya upande wa upinzani ambayo yamepangwa kuanza hapo kesho.Vikosi vya usalama vimepiga marufuku mikutano yote ya hadhara.