1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yapendekeza azimio kulaani machafuko Syria

Martin,Prema/ZPR16 Desemba 2011

Urusi imependekeza mswada wa azimio katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuhusiana na mzozo wa Syria.

https://p.dw.com/p/13Twl
epa02877427 Syrians converged on al-Hohafaza square in the heart of the capital Damascus, Syria on 22 August 2011. Reports state that the crowds gathered in support for President Bashar Assad, whose country has been gripped by more than five months of unrest. Assad said on 21 August 2011 in a televised interview that he is not worried and that the security situation is now better in the country. EPA/YOUSSEF BADAWI +++(c) dpa - Bildfunk+++ usage Germany only, Verwendung nur in Deutschland
Waandamanaji wanataka mageuzi ya kisiasa SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Bila ya kutazamiwa, Urusi imependekeza azimio hilo, kulaani mashambulio yanayofanywa na serikali ya Rais Bashar al-Assad na pia makundi ya upinzani. Nchi za magharibi katika Baraza la Usalama, zimekaribisha jitahada hiyo ya Urusi, lakini zimesema, mswada huo hata hivyo unahitaji kufanyiwa mabadiliko.

Wamekosoa kuwa machafuko ya wapinzani wa serikali ya Syria na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na serikali hiyo, vimewekwa katika kiwango kimoja. Vile vile, mswada huo haupendekezi vikwazo, kama wanachama wengi katika baraza hilo la usalama wanavyotaka.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema, nchi za magharibi zitajaribu kushirikiana na Urusi ili azimio la kwanza la Baraza la Usalama liweze kupitishwa kuhusu ukandamizaji unaoendelea Syria. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 5,000 wameuawa katika machafuko ya nchini humo.