1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatanua misuli yake katika mzozo wa gesi na Ukraine

CharoJosephat9 Januari 2009

Nani atakayekuwa mshindi katika mvutano huu?

https://p.dw.com/p/GV2p

Viongozi wa kampuni za gesi nchini Ukraine na Urusi wamekutana jana katika juhudi za kuutanzua mzozo wa gesi kati ya nchi hizo mbili. Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya nao pia umefanya mkutano mjini Brussels Ubelgiji kujadili mzozo huo huku wajumbe kutoka Urusi na Ukraine wakihudhuria.

Mzozo kati ya Urusi na Ukraine unauzifanya nchi hizo kubeba dhamana kwa usitishwaji wa ugavi wa gesi barani Ulaya. Urusi imesitisha usafirishaji wa gesi kwenda barani Ulaya kutokana na mzozo wa bei ya gesi ikidai Ukraine imeshindwa kulipa deni lake. Lakini mbali na mzozo huu kuna sababu nyengine; na kupimana nguvu huku kati ya Ukraine na Urusi kunaweza kutoa sura mpya ya waziri mkuu wa Urusi Vladamir Putin isiyotarajiwa.

Katika siku ya sita ya mzozo kati ya Urusi na Ukraine wa usafirishaji wa gesi katika nchi za Umoja wa Ulaya, waziri mkuu wa Urusi Vladamir Putini amenena wazi akisema sasa hatimaye Umoja wa Ulaya unatakiwa uwe umefahamu ilivyo muhimu na haraka kujenga bomba la kupitishia gesi kupitia bahari ya Baltic. Je kwa matamshi hayo Putin ametaja sababu halisi ya mzozo kati ya Urusi na Ukraine, ambao umesababisha matatizo makubwa katika nchi za Ulaya Mashariki lakini pia kuzusha hofu kubwa katika nchi za Ulaya magharibi?

Kutokana na uhuru huu wa Putin picha inayojitokeza ni hii: Ukraine inatakiwa ionekane kuwa nchi isiyoweza kutegemewa na nchi za Umoja wa Ulaya kama mahali ambapo gesi inaweza kupitia. Ili kutoweza kuitegemea tena Ukraine ambayo kutokana na mzozo huu si imara kisiasa, Umoja wa Ulaya utalazimika hatimaye kuamua kufuatilia ujenzi wa bomba kupitia bahari ya Baltic. Ndivyo hesabu zinavyopigwa wazi huko mjini Moscow.

Hata hivyo nchi tano wanachama wa Umoja wa Ulaya zikiwemo Sweden, Poland, jamhuri za zamani za Sovieti, Lithuania, Latvia na Estonia, zinapinga mpango huo. Sababu yao rasmi ya msimamo wao huo ni hatari za kimazingira zitakazosababishwa na bomba hilo. Katika kina cha bahari kuna mabaki ya silaha za kemikali za vita vya pili vya dunia na katika eneo hilo hilo bomba jipya la gesi linatakiwa kupitia.

Bila shaka serikali za nchi hizi tano zinaliona bomba hili kuwa chombo kinachotumiwa na utawala wa Urusi kushinikiza. Bomba hili litaifanya Poland kuwa nchi itakakopitia. Nchi hiyo itakuwa kama eneo la Baltic kuachanishwa kutoka kwa muungano wa nchi zinazotumia gesi barani Ulaya. Na nchi nne zilizosalia kutokana na hali hii zitakuwa chini ya shinikizo kutoka serikali ya mjini Moscow. Kwa njia ile ile inavyojaribu kuifanyia Ukraine.

Katika miaka iliyopita, Vladamir Putin hakuiweka siri kwamba serikali ya Moscow ingeitumia silaha ya nishati ikiwa Ukraine itaendelea kuikaribia miungano ya magharibi, Umoja wa Ulaya na jumuiya ya NATO.

Kwa kuwa idadi kubwa ya wanasiasa wa Ukraine wanaoegemea nchi za magharibi wanabeba dhamana kwa mzozo huu wa gesi, Ukraine kupitia utawala wake imekuwa mhanga wa siasa za ubabe za Urusi, uanachama wa Umoja wa Ulaya na jumuiya ya NATO kwa vyovyote vile hauko karibu. Zaidi ya hayo rais wa Ukraine Victor Yuschenko anayepigania mageuzi atasukumwa mbali na lengo la kuingiza Ukraine katika jumuiya hizo.

Mvutano kati ya Ukraine na Urusi hatimaye utamalizikia na ushindi wa gharama kubwa wa waziri mkuu Vladamir Putin. Katika nchi za Umoja wa Ulaya sauti zitazidi kusikika zitakazotaka uhuru kutokana na kutegemea nishati ya Urusi. Hii ina maana mzozo kati ya Urusi na Ukraine utamalizikia na kushindwa kwa pande zote mbili.

Ukraine itabakia nchi inayotumiwa kupitishia gesi isiyoweza kutegemewa na Urusi nayo itabakia kuwa nchi isiyoweza kutegemewa katika ugavi wa nishati ambayo mbali na hayo inatumia nishati zake kisiasa kuzilazimisha nchi jirani kuendelea kubakia chini ya ushawishi wake.

Mshindi anaweza kuwa Umoja wa Ulaya iwapo nchi wanachama hatimaye zitakuwa na mkakati wa pamoja wa nishati na nchi jirani za mashariki. Kwamba Urusi na Ukraine zimewaalika wachunguzi wa Umoja wa Ulaya, umoja huo ukijitokeza kama msuluhishi, ni hatua inayouongezea nguvu umuhimu wa umoja wa Ulaya. Umoja huo unatakiwa kutumia wakati huu kwa njia nzuri kabisa kadri inavyowezekana.