1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifaru vya jeshi la Israel vyashambulia Wapalestina

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXPy

Wapalestina 2 wameuawa na 7 wengine wamejeruhiwa baada ya vifaru vya jeshi la Israel kushambulia kundi la Wapalestina,kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.Msemaji wa majeshi ya Kiisraeli amethibitisha kuwa kundi la wanamgambo waliokuwa wakijitayarisha kurusha makombora lililengwa katika eneo la Beit Lahiya.

Inaaminiwa kuwa Wapalestina hao ni wanachama wa kundi la Hamas linalodhibiti Ukanda wa Gaza.Zaidi ya Wapalestina darzeni mbili wameuawa katika mashambulizi ya Israel katika kipindi cha kama majuma mawili yaliyopita.