1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Serbia na Kosovo kukutana tena.

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTGD

Vienna. Viongozi kutoka Serbia na Kosovo wanatarajiwa kufanya duru ya mwisho ya mazungumzo leo mchana kutafuta muafaka juu ya hali ya baadaye ya jimbo la kusini ya Serbia la Kosovo. Makundi hayo mawili yanakutana mjini Baden , nchini Austria kwa mazungumzo ya upatanishi unaofanywa na umoja wa Ulaya, Russia na Marekani. Mbali ya maajabu, mkutano huo unaofanyika katika hoteli ya Weikersdorf , unaelekea utamalizika bila ya kupatikana muafaka kwa kuwa pande zinazohusika zimebaki katika misimamo yao ambayo inapingana.Waziri mkuu mpya mtarajiwa wa Kosovo, kiongozi wa zamani wa waasi Hashim Thaci ameondoa uwezekano wa nafasi yoyote isipokuwa uhuru kamili kwa jimbo hilo.

Serbia imeweka wazi kuwa haitautambua uhuru wa jimbo hilo, lakini itakubali tu madaraka ya ndani ya jimbo hilo ambalo limekuwa katika utawala wa umoja wa mataifa tangu majeshi ya NATO yalipomaliza kampeni ya Serbia ya kuwaangamiza wakaazi wa jimbo hilo wenye asili ya Albania.