1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya kupambana na umasikini Umoja wa Ulaya

22 Januari 2010

Ifuatwe mikakati gani ?

https://p.dw.com/p/LdcC

Wajumbe mashuhuri wa Umoja wa Ulaya walifungua rasmi jana mjini Madrid, Spain, "mwaka wa Ulaya wa kupiga vita umasikini na kutowatenga wanyonge". Chini ya moyo "Si lazima kuwa masikini" ,wajumbe wanakusudia kuiweka mada hii hayi mwaka huu mzima .Wanasiasa wanaitisha vita dhidi ya ufukara na wanatilia mkazo umuhimu wa mazungumzo ya pande mbili-masikini na matajiri kwa masilahi ya mustakbala mwema barani Ulaya.

Kiasi cha wakaazi milioni 80 katika nchi za Umoja wa Ulaya, wanaishi katika hali ya umasikini. Na kima chao, ni sawa na 17 % ya wakaazi wote na hii ni aibu kwa muujibu asemavyo Rais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso.

Kwa hivyo, akawataka raia wa nchi za Umoja wa Ulaya, kujiwinda kupiga vita umasikini na amezitaka nchi zanachama wa Umoja huo, kufanya juhidi kubwa kupiga vita umasikini na kutengwa kwa wanyonge.Nae waziri-mkuu wa Spain ,Jose Luis Rodriguez Zapatero, ameahidi kuiunga mkono Kamisheni hiyo ya Umoja wa Ulaya katika vita vyake hivyo ilivyonadi:

"Kwa maana hiyo, kipindi hiki cha urais wa Spain ( Katika umoja wa Ulaya) kinaazimia kuvishughulikia maalumu vile vikundi vilio hatarini kutengwa pembeni. Vikundi vya wazee, walemavu na wasio na kazi , lakini pia wanawake. Nchi zote 27 zanachama, zinapaswa kuimarisha juhudi zao kupinga kutengwa pembeni umma wa watu wa aina hii."

Katika kikao hiki kilichoanza jana, wanasimulia pia hali zao masikini wenyewe au wanyongwe walioko kando ya jamii juu ya hali zao .

Kati yao ,ni bibi Marianna Poghosyan ambae miaka 4 nyuma, alihamia Valencia, Spain, kutoka Armenia.Anasimulia kuwa ,kuna matatizo mengi, na kwanza ni lugha, halfu humjui mtu , lakini si rahisi kuwa na mawasiliano na wenyeji. Huwezi tu kumwendea mwenyeji na kumwabia nimefika.

Kwa msaada lakini wa serikali, aliweza yeye na mumewe kujiunga na mafunzo ya lugha ya Kihispania, na hivyo akapiga hatua ya kwanza ya kujumuika na jamii.Waziri mkuu wa Spain, Zapatero, anadai kuwa, mipango ya kuwajumuisha wahamiaji na jamii, sera za nafasi za kazi inafaa kuboreshwa.

Kwa hivyo, ameahidi Spain, ikiwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya, itaisaidia Tume ya Ulaya, kutunga mikakati ya kusaidia ambayo itahimiza kuwajumuisha watu wa aina hii na jamii. Itaunga mkono pia kuanzishwa sheria ya kima cha chini kabisa cha mishahara. Halkadhalika, anapanga kukuza mabadilishano ya maarifa kati ya nchi za Umoja wa Ulaya.

Mwandishi: Spiegelhauer, Reinhard/Ali, Ramadhan/ZR

Mhariri: Miraji Othman