1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamana kuhusiana na mzozo wa taka.

8 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CmRZ

Napoli, Italia.Polisi wamepambana na mamia ya waandamanaji mjini Napoli usiku wa jana wakati mzozo wa kukusanya taka taka unaendelea. Wakaazi wa mji huo wameonekana wakijaribu kuzuwia juhudi za serikali za kufungua kwa muda dampo la taka nje kidogo ya mji wa Napoli. Taka zimelundikana katika mji huo ulioko kusini mwa Italia tangu pale magari ya kubeba taka yalipacha kufanya hivyo wiki mbili zilizopita kwasababu maeneo yote ya kutupia taka katika eneo hilo yamejaa. Jeshi la Italia limeanza kuondoa taka kutoka mashuleni na mitaano jana Jumatatu, wakati waziri mkuu Romano Prodi amesema kuwa atatangaza suluhisho la kudumu katika muda wa saa 24. Jimbo hilo limekumbwa na matatizo ya ukusanyaji wa taka kwa muda wa miaka 14.