1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi wa Arab League watakiwa kuondoka Syria

2 Januari 2012

Waandamanaji wanane wameuwawa Syria wakati Jumuiya ya Nchi za Kiarabu-Arab League ikitaka waangalizi wake waondoke nchini humo ikisema kuendelea kwa vitendo vya umwagikaji kunadhihaki mipango yao ya kurejesha amani.

https://p.dw.com/p/13clu
epa03046113 A handout picture released by Syrian Arab news agency SANA shows Arab League observers members wearing orange jackets checking the wounded people in the national hospital in Daraa, southern Syria, 31 December 2011. According to media reports on 31 December, Arab League peace observers, inspecting hotspots across Syria, have called on the government to remove 'immediately' snipers from rooftops of buildings. The observers are in Syria to verify the government's compliance with an Arab League peace plan, which includes removing military hardware from civilian areas and releasing detainees from prisons. More than 5,000 people have been killed in the Syrian government's crackdown on a pro-democracy uprising since it started in mid-March, according to the United Nations EPA/SANA HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waangalizi wa Arab LeaguePicha: picture-alliance/dpa

Vikosi vya ulinzi vya Rais Bashar al-Assad, vimekuwa vikidhibiti vikali maandamano makubwa mbele ya macho ya waangalizi wa nchi za kiarabu na kudaiwa kuuwa kiasi ya watu 286, tangu Desemba 23, siku moja kabla ya ujumbe wa waangalizi kutoka nchi za kiarabu kuwasili nchini Syria.

Kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu ambao wamekuwa wakifuatilia mikasa inayotokea nchini humo wamedai watu wanane waliuwawa kwa kupigwa risasi wakati vikosi vya ulinzi vilipowafyatulia risasi waandamanaji katika kiunga kimoja cha Damascus, Daria.

Bunge la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, chombo lenye wabunge 88 linye kuunganisha wawakilishi kutoka nchi za jumuiya hiyo limesema vurugu zinaendelea kuathiri watu wengi.

Mwenyekiti wake, Ali al-Salem al-Dekbas alisema kutokea kwa jambo hilo kunaongoza hasira kwa jamii ya Kiarabu na inakwenda kinyume na madhumuni ya kutuma ujumbe wa kutafuta ukweli nchini Syria.

Arab League Secretary General, Nabil al-Arabi, left, Qatari Prime Minister and head of state Hamad ben Jassem, center, and Ahmed bin Heli, the Arab League's assistant secretary-general for political affairs during the Meeting of the Committee of Ministers of the Arab League to discuss the situation in Syria held in Doha, Saturday, Dec. 17, 2011. (AP Photo/Osama Faisal)
Bunge la Arab LeaguePicha: AP

Kiongozi huyo aliendelea kwa kusema vitendo hivyo ni sawa na kutoa ridhaa ya kwa utawala wa nchi hiyo kuwafanyia maovu watu mbele ya masikio na macho ya Arab League.

Wapinzani wa Assad, waliukaraibisha ujumbe wa nchi za Kiarabu nchi humo ikionekana kama nafasi ya nadra sana kwa watu wa nje kuingia kushuhudia juu ya hali ya mambo yalivyo nchini humo. Lakini pia walikuwa na matumaini duni kama ujumbe huo ungeweza kufanikisha kuufikisha kikomo ukandamziaji ambao Umoja wa Mataifa unakadiria zaidi ya watu 5,000 kuuwawa tangu Machi.

Waangalizi hao nchini Syria wanafuatilia utekelezaji wa mpango wa amani wa Arab League  ambao unamtaka rais Assad kuondoa majeshi mitaani, kuwachia uhuru watu aliowatia kizuizini pamoja na kufungua milango ya mazungumzo na wapinzani.

Awali Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu,  Nabil Elaraby alisema itawachukua wiki moja tu kubaini kama Assad anatakeleza yale aliyoahidi.

Mpinzani, mwingine alisdema Rima Fleihan, kutoka Baraza la Kitaifa la Syria SNC alisema uwepo wa waangalizi hakujaathiri tabia ya utawala wa nchi hiyo ya kuendeleza mauwaji.

Waangalizi wa hao pamoja na maeneo mengine walitembelea mji wa Deraa eneo la mwanzo la vuguvugu la kumpinga Assad lilipoanza na kufika nyumbani kwa Sheikh Ahmad Hayasneh, imam mkuu wa msikiti wa Omari.

Msikiti huo ndipo kulipoanza maandamano ya awali ya kuupinga utawala wa Assad ingawa pia haijawa wazi kama kiongozi huyo alipatikana kwa kuwa inadaiwa kwamba amewekwa katika kifungo cha nyumbani kwa zaidi ya miezi mitano sasa.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR
Mhariri: Mohammed Khelef