1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi 48 wa Tamil Tigers wauwawa na jeshi la Sri Lanka

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6OT

Wanajeshi wa Sri Lanka wakisaidiwa na vifaru wamewaua waasi 48 wa Tamil Tigers na kuwajeruhi wengine 28 katika mapambano kadhaa kaskazini mwa nchi hiyo.

Jeshi la Sri Lanka limesema linaendelea kuzishambulia ngome za waasi hao.

Msemaji wa jeshi amethibitisha kwamba wanajeshi kumi wameuwawa na wengine 30 kujeruhiwa katika mapambanao hayo yaliyozuka jana katika eneo la Jaffna na wilaya za Vavuniya, Polonnaruwa na Mannar.

Waasi wa Tamil Tigers hawajasema lolote kuhusu mapigano kati yao na jeshi la serikali lakini wachambuzi wanasema pande zote mbili zinaiongeza idadi ya vifo kwa kutokuwepo na takwimu huru za wanaouwawa katika mapambano hayo.

Vita kati ya jeshi la serikali na waasi wa Tamil Tigers vimekuwa vikipamba moto tangu serikali ilipofutilia mbali mkataba wa kusitisha mapigano mwezi uliopita ambao ulikuwa umedumu muda wa miaka sita.

Serikali inasema waasi waliutumia mkataba huo kujihami tena.