1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wauzingira mji mkuu wa Chad

1 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D161

N’DJAMENA:

Shirika linalowahudumia wakimbizi la UNHCR limewaondoa watumishi wake kutoka maeneo ya Guereda mashariki mwa Chad kufuatia kutokea mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi.

Taarifa ya shirika hilo ambayo imetolewa leo,imesema kuwa watumishi wa shirika hilo wameshambuliwa mara kadhaa katika kipindi cha saa 72 zilizopita kutoka kwa watu waliovalia sare za kijeshi wakiingia katika maeneo yao na kuwatishia walinzi wao.

Taarifa zinasema kuwa magari yapatayo 300, ya waasi wanaoipinga serikali, yanakaribia mji wa N’djamena,yakiwa umbali wa kilomita 200 mashariki mwa mji mkuu.Mapema wiki hii, ndege za kijeshi za serikali, zilihujumu vituo vya waasi hao.Mashambulio mapya yamekuja wakati Umoja wa Ulaya ilipoidhinisha kutuma kikosi cha kulinda amani na kutumwa nchini Chad. Askari hao wa jeshi la Umoja wa Ulaya-wanaofikia 3,700 watawekwa kwenye mpaka wa Chad na Sudan ili kuwalinda wakimbizi wa Darfur.

Shirika la UNHCR limesema hata hivyo litabakiza wafanya kazi wachache katikaeneo hilo na waku wa kambi watasaidia kutoa chakula na maji kwa wakimbizi walioko huko wapatao elf 30.