1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Kiislamu kukutana na Rais wa Sudan

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVU5

Wabunge 2 wa Kiislamu katika Bunge la Malodi la Uingereza wamekwenda Sudan katika juhudi ya kupata uhuru wa mwalimu wa Kingereza Gillian Gibbons.Malodi hao wanatazamia kukutana na Rais wa Sudan,Omar al Bashir.

Siku ya Alkhamisi,mwalimu Gibbons alie na umri wa miaka 54 alipewa adhabu ya kifungo cha siku 15 kwa sababu ya kuwaruhusu wanafunzi wake kutumia jina la Mohamed kwa dubu la sanamu yaani „teddy bear.“Maelfu ya watu waliandamana mjini Khartoum siku ya Ijumaa na kudai kuwa mwalimu huyo apewe adhabu ya kifo.