1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wa Kisomali wakatiliwa kuingia nchini Kenya

5 Aprili 2007

Inasemekana karibu ya wakimbizi wa Kisomali 7,000 walioyakimbia mapigano mepya katika nchi yao ilio na vurugu wamekataliwa kuingia Kenya.

https://p.dw.com/p/CHGt
Wakimbizi wa Kisomali nchini Kenya
Wakimbizi wa Kisomali nchini KenyaPicha: AP

Wakimbizi hao wakiwa katika misafara ya ngamia na magari walikataliwa kuingia katika miji ya mipakani ya Afmadhow na Dobley pale walipotaka kuyafikia makambi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi, UNHCR,katika wilaya ya Garissa.

Saumu Mwasimba alizungumza na Mulicent Mutuli, afisa wa habari wa Shirika la UNHCR huko Nairobi, juu ya mkasa huo.