1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakosoaji wa rais Kais Saied wazidi kukandamizwa Tunisia

15 Februari 2023

Kukamatwa kwa viongozi wa kisiasa na vyombo vya habari kunaashiria awamu mpya ya mapambano baina ya Rais wa Tunisia na upinzani uliogawanyika lakini ulio na hamasa, na hivyo kuzua hofu ya kampeni ya kuzima upinzani.

https://p.dw.com/p/4NVhW
Tunesien I Protest gegen Kais Saed in Tunis
Picha: Yassine Mahjoub/NurPhoto/picture alliance

Tangu Rais Saied alivunje bunge miezi 18 iliyopita, na kuhamia kwenye utawala wa amri kabla ya kuandika upya katiba, vikosi vya usalama vilikuwa vikiwandama mara chache tu wapinzani wanaomtuhumu kwa mapinduzi na kujileimbikizia madaraka. Saied amekanusha tuhuma hizo akisema hatua zake zilikuwa halali na muhimu kuiokoa Tunisia kutokana na machafuko.

Aliahidi kuheshimu haki na uhuru vilivyopatikana kufuatia vuguvugu la mabadiliko la mwaka  2011 lililoleta demokrasia.

soma zaidi: Rais wa Tunisia awalaumu wafungwa kwa misukosuko ya nchi

Hata hivyo, wimbi la kamatakamata tangu Jumamosi iliyopita linaonyesha hatua mpya kali dhidi ya wakosoaji wa rais huyo na uchochezi kutoka kampeni ya shinikizo iliyoongezeka katika miezi ya karibuni kwa marufuku za kusafiri na uchunguzi.

Polisi wamewatia mbaroni wanasiasa wa upinzani, mfanyabiashara mwenye ushawishi, mkuu wa chombo muhimu zaidi huru cha habari, majaji mawili na afisa kutoka chama chenye nguvu cha wafanyakazi.

Usafiri wasimama Tunis, kufuatia mgomo wa watumishi

Wakati mamlaka bado haijazungumzia kukamatwa kwa watu hao, mawakili wa baadhi ya waliozuiliwa wamesema walituhumiwa kula njama dhidi ya usalama wa taifa. Mwanasheria wa Noureddine Boutar, mkuu wa kituo kikuu huru cha habari nchini humo cha Mosaique FM, alisema alikuwa akihojiwa kuhusu sera ya ufadhili na uhariri wa kituo chake cha redio, ikiwa ni pamoja na jinsi kilivyochagua wageni.

Waandishi habari wasema hawana uhuru wa kujieleza Tunisia

Tunesien  Tunis | Protest für Pressefreiheit
Waandishi habari waandamana Tunisia kutetea uwepo wa uhuru wa kujieleza nchini humo Picha: Chokri Mahjoub/ZUMA Wire/IMAGO

Kiongozi wa chama cha waandishi habari Mahdi Jlassi, alielezea hatari inayowakabili, na kusema ujumbe wa serikali kwa waandishi ambao hawajaingia katika hali ya utiifu ni kwamba hiyo ndiyo itakuwa hatma yao.

Wakosoaji wa serikali wakamatwa Tunisia

Ukamataji huo unakuja katika wakati muhimu kwa rais Saied. Uitikiaji mdogo wa asilimia 11 katika uchaguzi wa bunge ambao ni sehemu ya mfumo wake mpya wa kisiasa, ulitajwa na upinzani kama ushahidi kwamba mabadiliko ya rais huyo yanakosa uungwaji mkono wa umma.

Chama cha wafanyakazi cha UGTT kuchukuwa hatua za moja kwa moja dhidi ya Saied kuhusiana na mipango yake ya kiuchumi, kukataa kwake mapendekezo ya chama hicho kwa ajili ya majadiliano ya kisiasa, na kukamatwa mwezi uliopita kwa mmoja wa maafisa wake wa juu.

Upinzani Tunisia wasema polisi walijaribu kuzuia mkutano

Juhudi za kupata mkopo wa nje kwa ajili ya hazina ya taifa zimekwama, huku mashirika ya viwango yakisema Tunisia iko katika hatari ya kushindwa kulipa madeni baada ya mzozo wa kiuchumi kusababisha uhaba.

Kimataifa pia Tunisia inaonekana kutengwa zaidi, msaada wa magharibi ukiwa umepungua pakubwa, hakuna dalili ya msaada kutoka mataifa ya Kiarabu ya Ghuba, na mzozo mpya wiki iliyopita na mshirika wake mkuu na jirani Algeria.

Wakati huo huo kiongozi wa upinzani Nejib Chebbi, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba makundi ya upinzani uliogawika kwa muda mrefu yameanza kuzungumza kuhusu njia za kuweka kando uhasama wao wa zamanai ili kushirikiana dhidi ya Saied.

Wakosoaji wahofia demokrasia huenda ikatoweka kabisa

World Press Freedom Day | 2013 Tunesien
Maandamano ya kutaka mabadiliko yazidi kuongezeka TunisiaPicha: Mohamed Messara/Epa/dpa/picture alliance

Wakosoaji wa Saied wanahofia kukamatwa huko kunamaanisha kuwa matamshi yake makali ya kuwalamu mahasimu kama wasaliti yanaingia katika hatua kali zinazowezeshwa na kujilimbikizia mamlaka, ikiwa ni pamoja na dhana yake mwaka jana ya kuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mahakama.

Mwanaharakati wa Tunisia Khayam Turki akamatwa na polisi

Wana wasiwasi kuhusu hatua zake dhahiri za kulisogeza jeshi karibu na serikali, kama ilivyodhihirika katika uteuzi wake wa afisa mkuu wa jeshi kuwa waziri wa kilimo mwezi uliopita.

Wakosoaji pia wanataja matumizi yanayoongezeka ya mahakama za kijeshi ili kusikiliza kesi za kisiasa tangu Saied aliponyakua madaraka mwaka 2021. Serikali za nyuma pia zilitumia mahakama za kijeshi lakini mara chache sana. Hata hivyo wachambuzi wanasema hakuna dalili kwamba jeshi linatafuta kuwa na jukumu la kisiasa.

Chanzo: RTRE