1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wa kipalastina

Hamidou, Oumilkher23 Agosti 2008

Wanaharakati wa kipalastina wamepania kuvunja vizuwizi huko Gaza

https://p.dw.com/p/F3c3

Gaza:


Meli mbili zinazowasafirisha wanaharakati 44 wa kipalastina zinajongelea eneo la bahari la Gaza.Wanaharakati hao wamepania kuvunja vizuwizi vya Israel katika Gaza."Wanajongelea eneo la bahari la Gaza" amesema msem,aji wa tawi la Jerusalem la vugu vugu la kupigania ukombozi wa Gaza,Angela Godfrey-Goldstein.Amezungumzia hata hivyo shida za mawasiliano ya simu kati ya wanaharakati hao na wasimamizi wa opereshini hiyo.Katika taarifa yao iliyochapishwa hii leo,wanaharakati hao wameitolea mwito serikali ya Ugiriki na jumuia ya kimataifa wawajibike na kudhamini usalama wa raia wanaosafiri katika meli hizo zinazopita katika maeneo ya bahari ya kimataifa."Tunafuatilizia hali ya mambo,wanatafuta uchukozi tuu,tunajua jinsi ya kuzuwia jambo hilo" amesema kwa upande wake msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Israel Aryé Mekel.Israel imewaaonya wanaharakati hao wasiteterekee vizuwizi vilivyowekwa baharini dhidi ya Gaza.