1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi takriban 16 wa Pakistan wauwawa

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSgr

Mashambulizi mawili ya mabomu yaliyofanywa na watu wa kujitoa muhanga maisha dhidi ya wanajeshi yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 16 katika mji wa Rawalpindi, kusini mwa mji mkuu Islamabad nchini Pakistan.

Motokaa ya kwanza ililigonga basi lililokuwa limewabeba wanajeshi katika jengo la wakala wa ujasusi na kuwaua watu 13.

Mshambuliaji wa pili alikishambulia kituo cha ukaguzi karibu na makao makuu ya jeshi la Pakistan, karibu kilomita tatu kutoka eneo lililoshambuliwa kwanza.

Mashambulizi hayo yamefanywa majuma matatu tangu rais Pervez Musharraf alipotangaza utawala wa hali ya hatari nchini Pakistan.

Msemaji wa jeshi la Pakistan, meja jenerali Waheed Arshad, amethibitisha kuwa mashambulizi yote mawili yalikuwa ya mabomu yaliyokuwa ndani ya motokaa. Amethibitisha pia kwamba wanajeshi 15 wameuwawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya katika hujuma hizo.

Lakini maafisa wa usalama wamesema wanajeshi 19 wameuwawa kwenye shambulio dhidi ya basi na mmoja kwenye kituo cha upekuzi.