1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina wa Gaza

21 Januari 2009

Hali baada ya kuhama majeshi ya Israel gaza.

https://p.dw.com/p/GdmT
WapalestinaPicha: AP

Israel ilitangaza jana kuwa imekamilisha kuondoa majeshi yake kutoka Mwambao wa Gaza. Siku chache baada ya kila upande kutangaza kusima misha vita,raia wameanza kurejea maskani mwao huko Mwambao wa gaza mradi tu maskani hayo yapo.

Ngazi ya Bibi Umm Yassar imejaa vigae na taka.Angalia anasema mtoto wake wa kiume ,hapa umebakia uporo wa chakula waliokula wanajeshi wa israel.Unaona vibati vyenye maandishi ya kihebrew,mifuko ya vinwanyi na vipande vya mkate vilivyokauka.Baada ya kuivamia gaza ,vikosi vya Israel vilipiga maskani yao nyumbani mwa Umm Yassar.

"Kwanza ,walieeneza vipeperushi kuwa sote tutoke nyumbani mwetu.Kwahivyo, tukakimbilia katika shule ya Umoja wa mataifa."

Ni baada ya kusimamishwa mapigano Umm Yassar,alirejea kwake na kukuta nyumba yake imeporomolewa kabisa.Kuta za nyumba hazikuguswa lakini ndani kila kitu kimevunjwa.

"Hiki ni chumba cha kulalia mwanangu alieoa karibuni.Waisraeli wameteketeza kila kitu chumbani humu.Nyumba yetu haikufika hata miaka 7 tangu kujengwa.Hatukuweza hata kuifurahia."

Kabla ya kuondoka, wanajeshi wa Israel waliteketeza fanicha yote.Walibomoa hata tangi la maji lililokua juu ya paa la nyumba.ukoo huu wa watu 9 ukaanza kazi ya safisha-safisha.kurejea kuhamia nyumba hii bado hawako tayari,kwani wanadhani kutokana na kubomolewa kutakwa kupigwa risasi,huenda nyumba yao ikaporomoka.

Kiasi cha wakimbizi wa vita hivi 20,000 sasa wamerejea maskani mwao huko gaza-hii ni kwa muujibu wa shirika la misaada la Umoja wa mataifa UNRWA.Nusu ya idadi hiyo wanaendelea kuishi katika maskani za dharura na hasa mashuleni.

Kwa muujibu wa taarifa za UM ,wakaazi laki 1 wa Gaza hawana maskani.Abu Ahmad anaishihuko Tauwwam, mtaa wa Gaza.Hapa mlolongo wa vifaru vya Israel ulibomoa mtaa mzima na kiasi cha nyumba 50 zimezikwa kwenye vifusi.Mara tu vifaru hivyo vilipoondoka, wakaazi walirejea -asema Abu Ahmad,jirani wa Muhammad Wadi.

"Niimechimbua mawe yaliosalia nyumbani mwangu.Mwanangu alirekebisha kuta za nyumba na kuweka paa la mabati..Hapa tunakaa kutwa nzima.Hatuwezi kulala hapa ."-alinungunika mke wa Bw.Muhammad.