1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Warsaw.Chama tawala chataka kuandaa mpango wa serikali ya muungano.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD24

Chama cha kihafidhina chasheria za na haki nchini Poland, kimefikia makubaliano ya kurejesha tena muungano kati yao na vyama vya siasa kali vya mrengo wa kulia.

Rais Lech Kaczynski amempendekeza Andrzej Lepper kuwa makamo wa waziri mkuu, ikiwa ni wiki tatu tu baada ya Lepper kufukuzwa kazi kufuatia mabishano yake na waziri mkuu Jaroslaw Kaczynski, kaka wa Rais Lech.

Ufufuaji huo wa serikali umekuja siku moja tu kabla ya kikao cha Bunge ambacho upinzani unategemewa kuitisha kura ya kutokuwa na imani na kura nyengine ya kuitishwa uchaguzi mkuu mapema.