1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAWSuala la :Katiba mpya ya Umoja wa Ulaya kujadiliwa tena

20 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpz

Waziri mkuu wa Poland Jaroslaw Kaczynski amesema nchi yake haiwezi kuzuia mkataba mpya utakaochukua mahala pa katiba ya Umoja wa ulaya iliyokataliwa.

Poland na Ujerumani zimekuwa katika mvutano juu ya mfumo wa kupiga kura ambao kansela Angela Merkel ameupendekeza akiwa kiongozi wa Umoja wa Ulaya.

Katika mahojiano na gazeti la kila siku la Ujerumani la Bild Kaczynski amesema inachotaka nchi yake ni kuwepo mazungumzo kuhusu mfumo huo wa kupiga kura .

Kamishna wa Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso amezitolea mwito nchi zinazopinga makubaliano juu ya mageuzi kubadili msimamo wao katika mkutano wa kilele wa Umoja huo utakaofanyika kesho na keshokutwa mjini Brussels.