1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bunge la Marekani laidhinisha matumizi ya jeshi

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByT

Mabaraza yote mawili katika bunge la Marekani, yameidhinisha mswada wa kugharimia vita vya Iraq. Rais George W.Bush amesifu hatua hiyo ya maafikiano kati ya Wademokrat na Warepublikan ya kutopanga tarehe ya kuondosha vikosi vya Marekani kutoka Iraq.Wademokrat walitaka kufungamanisha mswada huo wa pesa pamoja na tarehe ya kuyarejesha nyumbani majeshi ya Marekani.Bush lakini hapo awali alipinga masharti hayo kwa kutumia kura ya turufu.Wabunge wa Demokrat,hawana wingi wa theluthi mbili unaohitajiwa,ili kuweza kuipinga kura turufu ya rais.Kwa upande mwingine Bush amesema,majuma yajayo nchini Iraq yatakuwa muhimu kwa mkakati mpya wa Marekani kuhusu usalama.Akaongezea kuwa anatarajia kuzuka kwa mapambano makali baada ya Marekani kuongeza vikosi vyake nchini Irak,ifikapo katikati ya mwezi Juni.