1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush akutana na makamanda wa jeshi

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0O

Rais George W Bush wa Marekani anakutana na makamanda wa jeshi katika ikulu yake hii leo.

Rais Bush amesema atafanya kila mabadiliko yanahitajika katika juhdui za kukabiliana na upinzani nchini Irak, lakini akaapa kutobadili lengo lake la kuunda serikali ya Irak itakayoweza kujitegemea.

Aidha Bush amekiri kwamba mashambulio nchini Irak yameongezeka sana wakati wa wiki za kwanza za mwezi mtukufu wa Ramadhani. Amesema kipindi hicho kimesababisha changamoto kubwa kwa majeshi ya Marekani yaliyo Irak na wairaki wote kwa jumla.