1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush awalaumu wanachama wa Demokratik katika Congress

4 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCf

Rais George Bush wa Marekani amelaumu wingi wa uwakilishi wa chama cha Demokratik katika bunge la Congress kuhusika na hatua ya kuishinikiza serikali itoe ratiba ya kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Irak pamoja na kusimamia kiwango cha fedha kinacho idhinishwa kwa ajili ya vita vya Irak na Afghanistan.

Bunge la Congres kwa sasa lina shughulikia kitita cha dola bilioni 96 kwa ajili ya kufadhili maeneo yanayokabiliwa na mizozo.

Rais Bush amesema mjini Washington kuwa kutokana na kuingizwa katika mswaada huo swala la kuwaondoa wanajeshi wa Marekani chama cha Demokratik kinapoteza muda wake bure.

Wakati huo huo spika wa bunge la marekani bibi Nancy Pelosi yuko mjini Damascus kwa mazungumzo na utawala wa Syria.

Ziara yake hiyo imezusha sintofahamu katika utawala mjini Washington na rais Bush amesema kuwa ziara ya bibi Pelosi inakiuka sera za nje za Marekani.