1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush azungumzia mabadiliko kuhusu mkakati wa Irak

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtV

Marekani inazidi kuashiria kuwa inajitayarisha kufanya mabadiliko makuu katika mkakati wake nchini Irak.Rais George W.Bush,katika hotuba yake ya kila juma kwenye redio amesema,waziri wake mpya wa ulinzi,Robert Gates ni mjumbe wa mabadiliko,atakaeleta mtazamo mpya juu ya njia za kushinda nchini Irak.Bush vile vile ameahidi kushirikiana na Wademokrat ili kuhakikisha ushindi katika vita vya Marekani vya kupambana na ugaidi.