1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yajizuwia kuamua juu ya hatima ya gereza la Guantanamo

13 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3C

Marekani imejizuwia kubainisha msimamo wake kuhusu pendekezo la serikali ya Uingereza la kutaka jela ya Guantanamo nchini Cuba ifungwe. Msemaji wa wizara ya maswala ya nchi za nje ya Marekani Sean Mc Cormarck, amesema Marekani inaangalia siku watafikia hali ya kufanya hivyo lakini kwa sasa, amezidi kusema kunazuwiliwa watu hatari. Jana waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Margaret Beckett, alitetea dai la kutaka gereza la Guantanamo lifungwe wakati alipokuwa akitoa ripoti ya kila mwaka kuhusu haki za binaadamu. Alisema kuwafunga watu bila kuwatendea haki kisheria ni jambo lisilokubalika kibinaadamu. Hivi karibuni Marekani kwa mara ya kwanza iliwaruhusu wafanyakazi wa Msalaba mwekundu kuwatembelea wafungwa 14 washukiwa wa kigaidi ambao walipelekwa katika jela hiyo ya Guantanamo mwezi uliopita. Miongoni mwa wafungwa hao waliotembelewa na Msalaba mwekundu kulikuwemo yule anayedaiwa na Marekani kuwa ndie alitoa muelekeo wa mashambulizi ya Septemba 11 mwaka wa 2001 Khalid Sheikh Mohammed.