1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mwanamke wa kwanza katika historia achaguliwa kuwa spika wa baraza la wawakilishi.

5 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCd9
Hayati Rafik Hariri
Hayati Rafik HaririPicha: AP

Nchini Marekani, Nancy Pelosi amekuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kuchaguliwa kuwa spika wa baraza la wawakilishi.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Democratic kutoka California alishinda kwa kura mia mbili na ishirini na tatu dhidi ya kura mia mbili na mbili.

Nancy Pelosi ametwaa wadhifa huo baada ya chama cha Democratic kuchukua udhibiti wa bunge kwa mara ya kwanza tangu miaka kumi na miwili iliyopita.

Chama cha Democratic kilishinda uchaguzi wa bunge wa mwezi Novemba kutokana na hali ya kukata tamaa ya raia wa Marekani kwa sababu ya jinsi utawala wa Bush unavyoendesha vita nchini Iraq.